Wakuu SADC waipongeza Tanzania, Rais Samia
- johnwengwi
- Aug 21
- 1 min read
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuimarisha amani na ulinzi katika eneo hilo.
Walitoa pongezi hizo baada ya kupokea taarifa ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Rais Samia kwenye mkutano wa 45 wa kawaida wa wakuu hao Antananarivo, Madagascar.
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango alimwakilisha Rais Samia katika mkutano huo.
Katika tamko la pamoja, wakuu hao wa nchi za SADC wameipongeza Tanzania kwa kuandaa kwa mafanikio mkutano wa Afrika kuhusu nishati Januari mwaka 2025, Dar es Salaam.




Comments