top of page
Search

Utalii Waivusha Tanzania Kwenye Kilele cha Mafanikio Chini ya Rais Samia

  • johnwengwi
  • 2 days ago
  • 1 min read

Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya utalii imepiga hatua kubwa na kufikia mafanikio ya kihistoria. Kupitia mikakati thabiti na ubunifu kama filamu ya Royal Tour iliyoitangaza Tanzania kimataifa, nchi imejipatia nafasi ya kipekee kwenye ramani ya dunia ya utalii.


Matokeo yameonekana kwenye ongezeko la watalii wa kimataifa kwa asilimia 132.1, kutoka 282,944 mwaka 2021 hadi 2,141,895 mwaka 2024. Watalii wa ndani nao wameongezeka kwa asilimia 307.9, kutoka 990,931 hadi 3,218,352 katika kipindi hicho, jambo linaloonesha hamasa kubwa ya wananchi kushiriki katika vivutio vyao.


Mapato kutoka utalii wa kimataifa yamepanda kutoka dola milioni 700 (sawa na TZS trilioni 1.82) mwaka 2021 hadi dola bilioni 3.9 (TZS trilioni 10.14) mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la TZS trilioni 8.32. Utalii wa ndani umeongeza mapato kutoka TZS bilioni 46.3 hadi TZS bilioni 209.8 katika kipindi hicho.


Kwa ujumla, ukuaji huu unaonyesha mchango mkubwa wa sekta ya utalii kwa uchumi wa Taifa chini ya Rais Samia. Kuongezeka kwa watalii na mapato kumeimarisha ajira, mapato ya Serikali na kuiweka Tanzania kama moja ya vivutio bora zaidi barani Afrika.


ree
ree

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page