top of page
Search

TANZIA: Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad Amefariki Dunia.

  • mwanzos12
  • Feb 17, 2021
  • 1 min read


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Mwinyi ametangaza kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, aliyefariki leo Jumatano Februari 17, 2021 asubuhi, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es salaam.

Ametangaza siku 7 za maombolezo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ambapo ametoa pole kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibar na wanachama wote wa ACT Wazalendo.


Pia Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza siku 3 za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kuanzia leo tarehe 17 Februari 2021 ambapo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.


Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad alizaliwa Oktoba 1943 kisiwani Pemba pia alikuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo . Aidha, amewahi kuwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page