top of page
Search

Tanzania Yapata simanzi, Kifo cha Rais Dkt.John Pombe Magufuli

  • mwanzos12
  • Mar 19, 2021
  • 1 min read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.


Taarifa za kifo cha Rais Magufuli, zilitangazwa Marchi 17, 2021 na aliyekuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alitangaza kifo akisema Magufuli alifariki dunia saa 12 jioni kwa maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Machi 6, 2021.


Alisema awali, Rais Magufuli alifikishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Machi 6 akisumbuliwa na tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10.


“Machi 14 mwaka huu, alijisikia vibaya akakimbizwa hospitali ya Mzena ambako aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hadi umauti ulipomkuta,” alisema Mama Samia.


Alisema Tanzania itakuwa katika kipindi cha maombolezo ya siku 21 na bendera zitapepea nusu mlingoti.


Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Libarikiwe 🙏🙏🙏.


 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page