top of page
Search

Simanzi Zatawala Katika Shughuli za Kuaga Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli

  • mwanzos12
  • Mar 25, 2021
  • 3 min read

Updated: Mar 26, 2021


Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan tangu tarehe 20/03/2021 hadi leo tarehe 26/06/2021 wanaendendelea na zoezi la kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifariki tarehe 17/03/2021 kwa tatizo mfumo wa umeme katika Moyo,ambalo alikuwa nalo kwa Zaidi ya miaka 10. Zoezi la kuaga linamalizika leo tarehe 26/03/2021 ambapo Mwili wa hayati Dkt. Magufuli utapumzishwa katika nyumba yake ya milele Wilayani Chato Mkoani Geita.

ree

Tarehe 20-21 /03/2021 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani aliwaongoza maelfu ya wakazi wa Dar es salaam kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli. Katika siku hizo mbili wakazi wa Dar es salaam walikusanyika katika uwanja wa Uhuru kutoa heshima zao za mwisho kwa hayati Magufuli, huku wananchi ambao hakuweza kufika katika uwanja huo walisimama pembezoni mwa barabara ambazo mwili ulikuwa ukipita kutoka/ kwenda hospitali ya Lugalo ulipohifadhiwa mwili wa Dkt. Magufuli. (Pichani ni Viongozi pamoja na baadhi ya wakazi wa Dar es salaam wakiaga mwili wa Dkt. Magufuli)


ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

Jioni ya tarehe 21/03/2021 Mwili ulisafirishwa kwenda Dodoma kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Ambapo kwa upande wa Dar es salaam wananchi waliusindikiza mwili hadi uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Dodoma mwili ulipokelewa katika uwanja wa ndege Dodoma na kupelekwa Ikulu ya Chamwino. Wananchi waliendelea kujitokeza barabarani kutoa heshima zao za mwisho, wakazi wa Dodoma walionekana kuwa na sura za huzuni na vilio.

ree

Tarehe 22/03/2021 ilikuwa siku ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli kitaifa, Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan aliwaongozwa viongozi wageni kutoka mataifa 17 walifika nchini kuaga mwili wa Dkt. Magufuli. Baadhi ya wageni wa nje waliofika kuaga mwili ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe.

ree
ree
ree
ree

ree

ree

ree
ree

ree

ree

Tarehe 23/03/2021 Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliwaongoza wakazi wa Zanzibar Kuaga Mwili wa Hayati Magufuli na baada ya kumaliza kuaga mwili ulipumzishwa Ikulu ya Zanzibar.

ree

ree

ree

ree


ree

ree

ree

ree

Tarehe 24/03/2021 Mwili uliwasili Jijini Mwanza ambapo maelfu ya wakazi wa Mwanza waliendelea kujitokeza barabarani kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli, Wananchi walijitokeza kuanzia uwanja wa ndege wa Mwanza mpaka Uwanja wa michezo wa CCM Kirumba. Vilio, kwikwi, watu kulala barabarani, kanga kutandikwa barabarani huku wengine wakiwa wameshika matawi ya miti pamoja na maua ndiyo ilikuwa taswira ya Mwanza katika kumlilia Marehemu John Magufuli, mwitikio ambao viongozi wa Serikali na waombolezaji wote uliwasisimua.


Baada ya kutoka katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, mwili wa Marehemu Dkt.John Pombe Magufuli ulipitishwa katika maeneo mbali mbali ya ndani na nje ya mji huo ili kutoa fursa kwa watu mbali mbali kutoa mkono wa kwaheri kwa hayati Dkt Magufuli.

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree


ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

ree

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 24/03/2021 ulivuka katika kivuko cha Kigongo-Busisi na kuelekea Chato mkoani Geita mara baada ya Wananchi wa Mwanza kupata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho.

ree

ree

ree

ree

Tarehe 24/03/2020 msafara huo ulianzasafari ya kwenda nyumbani kwake Chato mkoani Geita. Vilio na simazi vilitawala kwa wakazi wa Geita na tarehe 25/ wakazi wa Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla walipata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho ambapo ndiyo sehemu ya mwisho ya safari yake atakapohifadhiwa katika nyumba yake ya milele.


ree

ree

ree

ree

ree

ree

Tarehe 26/03/2021 ndiyo siku rasmi ya kupumsizsha mwili wa Magufuli, simazi na vilio vimeendelea kutawala miongoni mwa waombolezaji wote pamoja na waliofika Chato kushiriki kupumzisha mwili wa hayati Dkt. Magufuli.



Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe.

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page