top of page
Search

Rais Samia apewe Maua yake: Ujenzi wa Shule Maalum za Wasichana katika kila Mkoa nchini ndani ya miezi 48

  • johnwengwi
  • Aug 12
  • 1 min read

Tangu aingie madarakani ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameonesha kwa vitendo dhamira thabiti ya kuinua sekta ya elimu nchini. Kupitia sera, mipango, na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kielimu, Rais Samia amedhihirisha kuwa elimu si tu msingi wa maendeleo, bali pia silaha muhimu ya kuwawezesha Watanzania.


Moja ya mafanikio ya kujivunia ni mpango wa kujenga shule maalum za sekondari za wasichana zenye mchepuo wa sayansi katika kila mkoa wa Tanzania. Hii ni hatua ya kihistoria inayolenga kuziba pengo la kijinsia katika taaluma za sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati (STEM).


Mpaka sasa, shule hizi zimejengwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, na tayari wasichana zaidi ya 4,800 wamejiunga nazo, wakisoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Miundombinu iliyojengwa katika shule hizo ni ya kiwango cha juu, ikiwemo mabweni, madarasa, maabara za kisasa, maktaba, kumbi za TEHAMA, na nyumba za walimu.


ree

ree

ree


ree


ree

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page