Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kuaga Mwili wa Aliyekua Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Kijazi
- mwanzos12
- Feb 19, 2021
- 2 min read

Leo 19/02/2021 Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaongoza Watanzania kuaga mwili wa Marehemu Balozi John William Kijazi katika ibada iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Viongozi na wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam katika ibada ya kuuaga mwili wa Mwendazake Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Mwili wa Balozi Kijazi utazikwa Korogwe mkoani Tanga.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla walipokuwa wakitoa salamu za rambirambi baada ya ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.





Mwili wa Marehemu Balozi Injinia John Kijazi ukiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo shughuli za kuaga zinafanyika kabla ya kwenda Korogwe mkoani Tanga kwa mazi.




Fr. Dk. Joseph Matumaini akiongoza ibada ya kumuaga Marehemu Balozi Injinia John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es slaam leo Ijumaa Februari 19, 2021.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa kwa majonzi wakati mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi ulipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete wa pili kutoka kushoto, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mh. Hemedi Suleiman Abdallah kulia ni miongoni mwa waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Bashiru Ali na Waziri wa Sheria na Katiba Dk.Mwigulu Nchemba wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi Injinia John Kijazi.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Kamishna mkuu wa Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi kulia akiwa pamoja na Ndugu na jamaa wakati wa kuaga mwili wa ndugu yao mpendwa Marehemu Injinia Balozi John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akitoa salamu zake za rambirambi baada ya ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi.



Viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wametoa heshima zao za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi, shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. Baada ya shughuli hiyo mwili wa marehemu Kijazi umepelekwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa kupelekwa mjini Tanga-Korogwe kwa ajili ya mazishi hapo kesho tarehe 20 Februari, 2021.











Comments