Rais Dkt. Magufuli Azindua Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani ya Mbezi Luis
- mwanzos12
- Feb 24, 2021
- 1 min read











Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Februari 24, 2021 amezindua Stendi kuu ya mabasi ya Mikoani ya Mbezi Luis Jijini Dar es salaam. Stendi hiyo itaanza kutumika rasmi Februari 25, 2021 kwa magari kuanzia safari katika kituo hicho, na kituo cha mabasi cha Ubungo kilichokuwa kikitumika awali hakitatumika tena.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akikata utepe kuashiria Uzinduzi Rasmi wa Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Mbezi jijini Dar es salaam, kituo ambacho kitatumika na Wananchi, Mabasi yaendayo nje ya nchi na na yale yaendayo mikoani



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Hafla ya Uzinduzi Rasmi wa Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Mbezi jijini Dar es salaam. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 24 February, 2021 katika kituo hicho.
Wamachinga na wajasiriamali wadogo walipokuwa wakishangilia kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwaruhusu wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao katika stendi hiyo ambayo imezunduliwa leo.









Comments