top of page
Search

Rais Dkt. Magufuli Aweka Jiwe la Msingi wa Jengo Jipya la Soko Kuu la Kisutu

  • mwanzos12
  • Feb 25, 2021
  • 1 min read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo jipya la Soko Kuu la Kisutu katika Barabara ya Bibi Titi Mohamed jijini Dar es Salaam leo tarehe 25/02/2021.

Ujenzi wa Soko Kuu la Kisutu, Dar es Salaam lenye ghorofa sita umegharimu TZS bilioni 13.49. Soko hilo lina uwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 1,500, na pia litakuwa na maeneo ya huduma za kifedha na maegesho ya magari. Awali lilikuwa linahudumia wafanyabiashara 669.

Soko jipya la Kisutu linatarajiwa kukusanya hadi shilingi bilioni 2. 5 na zaidi huku likitoa ajira zaidi kwa vijana 2,000 hiki nacho ni kitu kizuri. Soko hili litabadalisha mandhari ya Jiji la Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla kwenye Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la msingi Soko la Kisutu Dar es salaam.

Mhe. Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa ‘’Nimeweka jiwe la msingi la Soko la Kisutu, ni kama nimemaliza kulifungua, mkandarasi hakikisha unalimalizia haraka maana lilipaswa liishe tangu mwaka jana, sasa umalize na kukabidhi tarehe ulizopangiwa. Inawezekana nikarudi tena kimyakimya kuja kuangalia kazi unayoifanya. Tumejenga masoko 22 Tanzania nzima, yapo yaliyokamilika na mengine yanaendelea kukamilishwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 119. 921 ili kumaliza changamoto zinazowakumba wakulima na wafanyabiashara’’.

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page