top of page
Search

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizindua Jengo la Jitegemee ambalo ni Studio za Africa Media Group

  • mwanzos12
  • Feb 25, 2021
  • 1 min read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Jitegemee zilizopo Studio za Africa Media Group ambazo ni Channel Ten, Channel Ten plus, Magic FM na Classic FM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam. leo Februari 25, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibofya kitufe kuzindua rasmi studio mpya za Channel Ten Plus TV, Radio Magic FM na Radio Classic FM katika jengo la Jitegemee.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli akifurahia wimbo wa "BABA" Wasanii Profesa Jay na Stamina wakati alipozindua rasmi studio za Channel Ten Plus TV katika jengo la Jitegemee.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea maeneo mbalimbali baada ya kuzindua rasmi jengo la Jitegemee House pamoja na Studio za Channel Ten Plus, Radio Magic FM na Radio Classic FM.

Katika hotuba yake Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa ''Natoa wito kwa watendaji wenzangu ndani ya Serikali kuwa wepesi katika kutoa taarifa, maana zipo Wizara ambazo zinaficha taarifa kwa waandishi wa habari. Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya habari fuatilieni hili, taarifa za maendeleo zitolewe mapema ili wananchi wajue ni lipi limefanyika. Serikali katika miaka mitano imeimarisha ipasavyo haki na wajibu wa vyombo vya habari na kuhakikisha vinatoa haki. Serikali haichukii wanaotupa changamoto na kukosoa kwa staha, kitakwimu tumeruhusu vyombo vya habari kuliko wakati wowote tangu tupate uhuru.''


ree


 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page