top of page
Search

NCHI ZA AFRIKA KULETA SAMPULI ZAO KUCHUNGUZWA TANZANIA

  • tumsifukabunduki
  • Mar 8, 2021
  • 2 min read

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema kuwa kutokana na umahiri wa maabara zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zimeweza kutoa huduma ya upimaji wa sampuli mbalimbali kutoka Katika nchi tofauti za Afrika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA ,Adam Fimbo katika mkutano maalum na waandishi wa habari kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo Dar es salaam kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo . Amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa na utaratibu wa kukagua na kuthibisha umahili wa maabara mbalimbali Duniani ambapo kwa nchi za Afrika Tanzania ni moja kati ya nchi chache iliyothibitishwa kuwa na maabara zenye ubora hivyo kupelekea baadhi ya nchi za Afrika kuleta Sampuli zao kwaajili ya kuchunguzwa. "Kuna viwango vilivowekwa na WHO ukifika hicho kiwango wanakutangaza na kukupa cheti hivyo kupelekea nchi nyingine kutaka kujifunza na kuleta Sampuli zao" amesema Fimbo. Ameongeza kuwa Nchi hizo ni pamoja na Zambia, Lesotho, Malawi, Uganga na Kenya na kwamba hilo limewezekana kutokana na tangazwa na WHO. Ziara hiyo ya siku tatu imehitimishwa rasmi Machi 5,2021 kwa waandishi wa habari kutembelea maabara ya Dawa na Vifaa Tiba nyongeza kwa kuangalia maabara maalumu ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa.


ree

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo kwenye Ofisi zao Dar es Salaam. kushoto Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza.

ree

Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza (kushoto) akizungumza na waandishi wakati wa kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu kuzungumza na waandishi hao.

ree

Mchunguzi wa Maabara TMDA,Gerald Sambu akufafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembea Maabara hiyo Dar es Salaam.

ree

Mchunguzi wa Maabara wa TMDA Olson Mkeya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika Maabara Maalum ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa.

ree

Waandishi wa habari wakimsiliza Mchunguzi wa Maabara TMDA, Gerald Sambu wa (kulia) Dar es Salaam.

ree

kazi ikiendelea

ree

Muonekano wa Maabara hiyo.

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page