Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Wazikwa Nyumbani Kwao Chato
- mwanzos12
- Mar 26, 2021
- 1 min read
Leo tarehe 26/03/2021 Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli umezikwa nyumbani kwao Chato Mkoani Geita.
Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wameambatana na Viongozi wastaafu Kupumzisha Mwili wa Hayati Dkt.John Pombe Magufuli. Ambapo kabla ya kumpumzisha walishiriki katika ibada ya kagame Mwili iliyofanyika katika Uwanja wa mpira wa Magufuli kijijini Chato.
Waombolezaji sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wameendelea kugubikwa na sura za simanzi na majonzi kwa kuondokewa na kiongozi makini na shupavu ambaye walitamani asiondoke wakati huo.
Kwa ujumla viongozi wakuu wa Serikali pamoja na waombolezaji wameeleza kuwa watamkumbuka daima Hayati Magufuli kwa usubutu wake wa kuongoza nchi pasipo kumuogopa mwanadamu mwezie.
Pichani ni wanafamilia wa Dkt. Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiweka maua kwenye Kaburi mara baada ya kuzika.
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani.

































Comments