Mradi wa Maji wa Bilioni 36.9 kuwanufaisha wakazi zaidi ya 450,000 Jijini Dar es Salaam
- johnwengwi
- Aug 13
- 1 min read
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 36.9 katika Mradi mkubwa wa Maji wa Bangulo—ukiwa ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya maji safi na salama.
Mradi huu unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, DAWASA, na unalenga kuhudumia wakazi wa maeneo ya Kusini mwa Jiji la Dar es Salaam.
Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ulazaji wa bomba kubwa la chuma lenye kipenyo cha inchi 28 kutoka Kituo cha Kusukuma Maji cha Kibamba hadi Bangulo, sambamba na ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi maji lenye uwezo wa lita milioni 9.
Mradi huu unaotarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ambapo unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi 450,000kwa kuwapatia huduma ya uhakika ya maji safi, salama na endelevu.



Comments