top of page
Search

Matukio Mbalimbali Wakati wa Kuaga Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif

  • mwanzos12
  • Feb 18, 2021
  • 2 min read

Updated: Feb 19, 2021


Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, umeagwa mapema leo asubuhi katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

Dua maalum imeongozwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi, ambapo Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Jakaya Kikwete aliongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa Maalim Seif Sharif Hamad Dar es salaam.

Helikopta iliyobeba mwili wa Maalim Seif Sharif Hamad (77), aliyefariki jana Jumatano ikiwa tayari kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa maziko yanayofanyika leo Alhamisi, Pemba.

Wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Unguja kusubiri mwili wa Mwendazake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad. Baada ya swala, mwili huo utasafirishwa kwenda kisiwani Pemba kwa ajili ya mazishi leo jioni katika eneo la Mtambwe.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Sala Maalum ya Kusalia Mwili wa  aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad iliyosaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo



Mwili wa Marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ukishushwa katika Helikota ya JWTZ baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ukitokea Jijini Dar es Salaam Leo.

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi wa pili kushoto mbele akiwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali na Chama wakati wa kuupokea mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad,ulipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amari Karume Jijini Zanzibar.

Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ukiwasili Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page