top of page
Search

MAKATIBU WAKUU SADC WAENDELEA NA KIKAO MKOANI DAR ES SALAAM

  • tumsifukabunduki
  • Mar 10, 2021
  • 1 min read

Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wameendelea na kikao chao kwa siku ya pili ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa baraza la mawaziri wa SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 – 13 Machi, 2021 kwa njia ya mtandao Mkoani Dar es Salaam.


Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho unaongozwa na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban.


Mkutano wa Baraza la Mawaziri ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ataongoza ujumbe wa Tanzania.


Mwenyekiti wa Sasa katika Jumuiya ya SADC ni msumbiji na ndiye atakayeongoza majadiliano ya Mkutano huu.


ree
ree
ree

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachoendelea jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakafanyika tarehe 12 – 13, Machi 2021 kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.

ree

ree

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page