top of page
Search

KOFFI OLOMIDE: NITAENDELEA KUWA KARIBU NA WATANZANIA

  • tumsifukabunduki
  • Feb 15, 2021
  • 1 min read

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na mwanamuziki galacha duniani katika muziki wa rhumba, Koffi Olomide aka Mzee ya Mboka, walipokutana usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam ambapo mwanamuziki huyo alikuwa nchini kutumbuiza chini ya mwaliko wa kampuni ya Prime Time Promotions na Clouds Intertainment.

Dkt. Abbasi alitumia muda huo kumshukuru mkongwe huyo kwa kuitangaza Tanzania mara kwa mara ikiwemo kushirikiana na wanamuziki vijana wa hapa nchini kuinua na kuutangaza muziki wao. Koffi aliahidi kuendelea kusaidia kukuza vipaji vya Tanzania akisema: "Dar es Salaam na Tanzania mimi ni kama nyumbani, nitaendelea kuwa nanyi karibu."

ree

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha mbalimbali na Mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyekuwa akitumbuiza katika tamasha la Mahaba ya Rhumba Jijini Dar es Salaam.

ree

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akimsikiliza Mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyekuwa akitumbuiza katika tamasha la Mahaba ya Rhumba Jijini Dar es Salaam.

ree
ree

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akimueleza jambo Mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyekuwa akitumbuiza katika tamasha la Mahaba ya Rhumba Jijini Dar es Salaam.

 
 
 

Comments


UntitledPost (5).jpg

MwanahabariOnline

GAZETI LA KILA MWEZI 

Powered by

Diaspora

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter

© 2025

bottom of page